Wazazi wameshauriwa kutowashinikiza wanao kupata gredi fulani zinazohitajika ili kujiunga na chuo kikuu. Mtaalam wa taaluma Caroline Gaithuma anasema hii inaweza kuwapa wasiwasi na kuathiri gredi zao.

juu kupita kiasi vya sumu ya aflatoxin. Kampuni hizo hata hivyo zinasema viwango vya sumu hiyo hutofautiana kutoka kwa maabara moja hadi nyingine na kusema kuwa wanataka kufanya uchunguzi wao wenyewe kisha walinganishe na matokeo ya KEBS.

Wamiliki wa kadi za hazina ya NHIF ambao hutegemea hospitali za kibinfasi katika maeneo ya mashinani huenda hivi karibuni wakakosa kupata huduma za matibabu. Shirika la hospitali za kibinafsi katika maeneo ya mashinani linasema huduma katika hospitali za kibinfasi zinazidi kulemezwa kutokana na hazini hiyo ya NHIF kutolipa madeni yako kwa hospitali hizo.

Mwanamme mmoja anapokea matibabu katika hospitali ya Kenyatta baada ya madaktari kufaulu katika kuondoa risasi saba mwilini mwaka baada ya kuvamiwa siku ya jumanne. Richard Mwema alipigwa risasi na Majambazi waliloliiba duka la Mpesa huko Kasarani alipojaribu kupigana nao.

Naibu gavana wa Taita Taveta Majala Mlagui amewaonya wahudumu wa afya dhidi ya kuanza mgomo wao ambao umepangiwa kuanza hapo kesho. Anasema tayari serikali inaendelea kutekeleza makubaliano ya awali kuhusu mishahara na marupurupuna na kuwa mgomo huo utaathiri juhudi za serikali za kuafikia matakwa ya wafanyikazi hao.

Tayari miungano sita ya wafanyikazi wa sekta ya afya wametishia kusitisha shughuli zao kuanzia kesho ili kuishnikiza serikali kuwalipa marupurupu.

Sio utumwa wa kuwajibika kwa mpenzi wako. Mshauri Patrick Masiga anasema kuwa wazi na mpenzi wako husaidia kuwepo kwa uaminifu katika uhusiano wenyu.

Wazazi wameshauriwa kutowashinikiza wanao kupata gredi fulani zinazohitajika ili kujiunga na chuo kikuu. Mtaalam wa taaluma Caroline Gaithuma anasema hii inaweza kuwapa wasiwasi na kuathiri gredi zao.

View Comments