TlMpZqOudlnt

Rais mtaafu Daniel Toroitich Arap Moi amerejeshwa hospitalini siku mbili baada ya kutolewa humo.

Msemaji wa familia Lee Njiru amesema kuwa amefikishwa hospitalini ili kupata uchunguzi wa kawaida wa afya yake.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Lee amesema kuwa umma utajulishwa jinsi matibabu yanavyoendelea.

“Naomba vyombo vya habari zisiweze kuhusika katika kukanganya na kuzua sintofahamu miongoni mwa raia.Tutatoa taarifa za matibabu jinsi muda unaposonga iwapo tutakiwa kufanya hivyo..." Amesema Lee Njiru

Aidha, Njiru amehakikishia wakenya kuwa afya ya Moi ni imara na anashughulikiwa na wataalam wa afya wanaoongozwa na David Silverstein.

Hii ni mara ya tatu Moi kupelekwa  hospitalini katika kipindi cha miezi miwili.

Ila je, ni tatizo gani madaktari wanachunguza?

Madaktari walisema kuwa Moi alikuwa na matatizo ya kifua yaliyotatiza kupumua.

Uchungu uliopo kwenye goti lake pia ni kati ya maswala na ambayo madaktari wanachunguza.

Tatizo la goti lilianza 2006 baada ya kuhusika ajali Limuru.

Mwezi wa Machi 2018, Moi alipelekwa Israel kuhusu matatizo ya goti lake.

Tarehe 27 Januari, 2017, Moi alifanyiwa upasuaji wa goti katika hospitali ya Agha Khan University Hospital hapa jijini Nairobi.

Moi alichukua hatamu ya uongozi wa taifa hii baada ya muasisi wa taifa hili Hayati Jomo Kenyatta kufariki.

Damu ya kisiasa ya Moi ilichemka baada ya kuzamia siasa 1955.\

Hii ni baada ya kuchaguliwa katika Legco kuwakilisha ukanda wa bonde la ufa

View Comments