Kiungo wa Liverpool Mohamed Salah atakosa mechi ya Misri ya kufuzu kwa AFCON dhidi ya Kenya na Comoros kwa kuwa ana jeraha la mguu. Salah aliungana na timu hio jijini Cairo jana ili kufanyiwa uchunguzi wa jeraha hilo.

Salah alikosa mechi ya Liverpool waliyotoka sare na Manchester United mwezi Oktoba baada ya kugongwa na Hamza Choudhury wa Leicester. Meneja Jurgen Klopp, aliyekasirishwa na Choudhury anasema Salah bado alikua akiuuguza mguu huo kabla ya kugongwa tena. Mechi ifuatayo ya Liverpool itakua ugenini dhidi ya Crystal Palace Novemba tarehe 23.

FKF jana ilizindua mkataba wa ufadhili wa shilingi milioni 90 na kampuni ya kamari ya Betika. Kufuati hili ligi ya daraja la pili humu nchini sasa itajulikana kama  Betika Super League kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo. Kwa mujibu wa masharti ya mkataba huu timu zote 20 katika mashindano hayo zitapokea ufadhili wa shilingi elfu 750 kila msimu. Vlabu hivyo pia vitapokea vifaa vingine vya soka.

Bingwa wa mbio za Marathon duniani Brigid Kosgei ni mmoja kati ya wanariadha watano wa kike waliorodheshwa kuwania tuzo la mwanariadha bora zaidi wa kike duniani, mwaka huu. Mwezi uliopita Kosgei aliipiku rekodi ya muingereza Paula Radcliffe ya miaka 16 kwa kukimbia kwa muda wa masaa mawili dakika 14 na sekunde nne na kushinda mbio za Chicago Marathon.

Kosgei pia alikua mshindi mchanga zaidi wa mbio za London Marathon mwezi Aprili. Wanariadha hao wegine ni pamoja na mwamerika  Dalilah Muhammad, mjaamaica Shelly-Ann Fraser, raia wa Venezuela Yulimar Rojas na wa Uholanzi  Sifan Hassan.

View Comments