- download
- 61ee6a9f_036c_4ad4_b5e2_35007202e13d__1573724492_65881

Aliyekuwa mpenzi wa Paul Manyasi amefunguka A-Z kumhusu.

Irene amesema kuwa Paul alipotea kazini na kuambiwa na msimamizi kuwa ibaki siri hadi arudi.

Irene anadaiwa kuwa mpenzi wake Paul.

Haya yanajiri huku shirika la ndege la Kenya Airways likikana taarifa za kuwa alikuwa akihudumu katika shirika hilo.

'Babake' Isaac anakana kuwa kijana huyo ni mwanawe.

Kizungumkuti kinazingira swala nzima huku wazazi' wakikataa ombi la kuendea mabaki ya mwili wa kijana huyo.

Kisa cha mwili wa Paul Manyasi kuanguka kutoka kwa ndege la shirika la KQ kiliwatia wengi hofu kubwa.

Kijana huyu anadaiwa kuwa mfanyakazi wa kusafisha katika kampuni ya Colnet.

Mpenzi wake kwa jina Irene amefunguka kuhusu usuhuba wao.

"Nilimpenda tu jinsi alivyokuwa. Tulikuwa katika makubaliano kuwa itafika siku tuoane. Nahisi kuwa nilipoteza kipenzi cha roho..."

Kampuni hii ya Colnet ilikuwa katika kandarasi ya kudumisha usafi katika uwanja wa ndege wa KAA.

Mwanadada huyu kwa jina Irene alisimulia jinsi alivyojaribu kumpigia simu bila yeye kuipokea.

"Niliipiga simu yake ila sikumpata na ilikuwa imezimwa. Msimamizi wetu kazini alimuulizia akamkosa..." Alisimulia Irene

View Comments