Diamond, Tanasha wanahatarisha kufungwa jela Tanzania
Staa na nguli wa muziki Afrika Diamond Platnumz na Tanasha Donna huenda wanahatarisha kutiwa nguvuni na mamlaka nchini Tanzania katika kipengele kipya cha kuhalalisha ndoa.
Nchi jirani ya Tanzania inasukumia kuwepo na urasmi wa ndoa kati ya raia wao.
Diamond na Tanasha ni miongoni mwa wanandoa nchini humo ambao hawajaona rasmi.
https://www.instagram.com/p/B4hsCzKAXnU/
Serikali ina mtazamo kuwa mtindo wa wanandoa kuishi chumba kimoja bila kuoana rasmi ni chanzo cha watoto wanaorandaranda mitaani.
Ndoa hizi zikivunjika, watoto hupata tabu kubwa sana na wengi huishia kuombaomba kwenye vichochoro.
Andrea TSele alitangaza kuwa wanandoa kama hao wakamatwe na kutiwa nguvuni ili wajue ubora wa kufunga ndoa.
TSele alikuwa akizungumza katika kata ndogo ya Mavanga jimbo la Ludewa Njombe .
Kinachomkera TSele ni wanaume wanaowakimbia wamama baadaye ya kuwatunga ujauzito.