75231806_719626555194490_266650042390020096_o-696x574

Afisa wa KCB (Kenya Commercial Bank) amepatikana amefariki chumbani baada ya kukosa kuonekana kazini.

Inadaiwa kuwa simu yake haikuwa inapokelewa alipopigiwa.

George Kiarie,ambaye ni meneja wa benki ya KCB tawi la Nanyuki alikosa kufika kazini Jumamosi.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi kaunti ya Nanyuki, Maxwell Nyaema mmoja wa wafanyakazi alishuku tukio hilo na kuandikisha kauli katika kituo cha polisi.

Kamanda huyu amesema kuwa maafisa wa polisi walifika kwake Immanuel Flats viunga vya Nanyuki na kuvunja mlango.

Walipata mwili wake kando ya choo.

 Kamanda wa polisi amesema kuwa wanafanya wawezalo kuhakikisha kuwa wamebaini kilichomuua meneja huyu.
 Mwili wa marehemu umelazwa katika hospitali ya rufaa ya Nanyuki.
Wengi walitoa risala zao katika mitandao ya kijamii
Margaret Kichi Gitonga: inaudhi sana. mungu ailaze roho yake pema peponi.

Esther Wambugu: habari za kuhuzunisha, tumepoteza mtu mwema.apumzike katika pahali pema. Mungu alinde familia.

Faith Basiye: inaudhi zaidi