Mfarakano na ubinafsi unaoshuhudiwa baina ya viongozi kutoka jamii ya Waluhya haswa kabla na baada ya uchaguzi mdogo wa Kibra, utawanyima nafasi ya uongozi wa kitaifa.

Kauli hiyo imesemwa na mbunge wa Garissa Township Aden Duale.

Duale ambaye pia ni kiongozi wa walio wengi katika bunge la kitaifa alisema kwamba iwapo viongozi katika jamii hiyo hawatasuluhisha tofauti zao, kupata madaraka ya kitaifa ni ndoto.

"Mgombeaji wa chama cha ANC alipata kura 5,000 huku mgombeaji wa Ford Kenya akipata kura 260. Hii ni ishara kwamba jamii ya Luhya inakumbwa na mfarakano. Iwapo wangechagua mgombeaji moja na kumuunga mkono, mambo yangekuwa tofauti," Duale alisema.

Mbunge huyo aliwarai jamii ya Waluhya kumuunga mkono Naibu wa Rais William Ruto ambaye "ana hatua moja tu afike kileleni."

Kinara wa ANC Musalia Mudavadi, Moses Wetangula wa Ford Kenya na gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya wote hao wameonesha azma ya kuwania kiti cha urais 2022.

Duale alisema hayo wikendi katika halfa ya kuchangisha pesa katika jamii ya Uislamu ktika kituo cha kibiashara cha Kimwanga, eneo bunge la Bumula.

Aidha alimpigia upato Ruto huku akisema azma yake ya kuingia ikuluni haitasimamishwa na yeyote.

Aliwatahadharisha dhidi ya ubinafsi na mgawano baina ya viongozi wa Mulembe kuwa itawazuia kufanikisha malengo yao.

Mbunge wa Bumula Mwambu Mabonga aliahidi kumpigia kampeni Naibu wa Rais William Ruto hadi atakapopata uongozi wa ki+

taifa.

View Comments