- WAKO.3.jfif
- WAKO.1.jfif
- WAKO.2.jfif

Aliyekuwa mwanasheria mkuu Amos Wako amepuuzilia mbali marufuku ya kuzuru Marekani.

Wako amabye ni seneta wa Busia alitaka Amerika kuweka wazi sababu zilizopelekea yeye kupigwa marufuku ya kusafiri nchini humo.

Wako alisema lengo la marufuku hiyo dhidi yake na familia yake ni kumharibia tu jina.

"Madai haya hayasaidii katika vita dhidi ya ufisadi. Ikiwa Marekani imejitolea kushirikina na nasi  katika vita dhidi ya ufisadi, wacha wanieleze mimi na wakenya wengine bayani madai dhidi yangu," alisema.

Wako alisema kwamba anauhakika na maadili yake na hana jambo la kuficha.

Alisema kwamba familia yake haikuwa ikifanya kazi naye akiwa mwanasheria mkuu na haifai kujumuishwa katika marufuku hiyo.

“Hata kama nilifanya dhambi, tuseme nilifanya ingawa sijafanya lolote, ningewajibikia makosa hayo bila kuhusisha mke wangu na mwanangu. Watu wa familia yangu hawafai kuadhibiwa kwa makosa yangu." Wako alisema.

Alisema kuweka mke na mwanake ni makosa.

“sijifanyi kuwa Yesu kujitoa kafara kwa makosa ya wengine. Mimi ni mkenya tu wa kawaida, niadhibiwe kwa makosa yangu".

Wako alithibitisha kwamba amekuwa akizuru Makekani licha ya marufuku ya mwaka 2009,

Seneta huyo alisema hapakuwepo na umuhimu wa kutoa marufuku hiyo kwa sababu ilikuwa tayari ishatolewa miaka 10 iliyopita.

View Comments