ma DJ

Watangazaji mahiri humu nchini, Mbusii na Lion deh wanatambulika humu nchini kwa kazi yao safi wakiwa hewani na pia nje mitaani wakitangamana na mamilioni ya mashabiki wao.

Kile wengi hawajui ni kuwa magwiji hao wawili wana shule ya kuwafunza DJs na pia MCs, ijulikanayo kama Hakuna mbrr entertainment. Lengo lao kuu ni kuwapa wakenya ambao wangependa kuingia katika usanii, mafunzo ya hali ya juu ili waweze kujikimu kimaisha.

Shule hiyo imekuza vipaji chungu nzima na baadhi ya ma DJ ambao wamehitimu, wao huwapa fursa kuonesha umahiri wao katika shoo yao ya Mbusii na Lion teketeke.

Kando na hilo, watangazaji hao kwanzia mwezi wa Oktoba wamekuwa wakiwasaidia ma DJ kutoka sehemu mbalimbali humu nchini kujiuza kupitia kipindi hicho ambacho hujia kuanzia mida ya saa tisa mchana.

"Chenye tumekuwa tukifanya, ma DJ huwa wanatuma mix zao na tunazicheza  kisha tunawapatia mashabiki fursa ya kuchagua ni yupi aliyewapendeza." Alisema Mbusii.

Aliongeza,

Hili tulianza Oktoba na huwa tunafanya hivi kila IJumaa na tunapania kwenda hadi Disemba. Kila mwezi sisi huchagua ma DJ watatu bora."

Upande wake Liondeh alisema kuwa mpango wao ni kuwa na kipindi katika runinga kuanzia Januari mwakani, kitakacho jumuisha DJ wenye watachaguliwa na mashabiki.

"Baada ya kuchaguliwa tutawaleta pamoja na watashinda moja kwa moja na atakayeshinda basi atajishindia nafasi ya kuungana na ma DJ wetu hapa studioni." Alisema Liondeh.

Cha kufurahisha ni kuwa kama watakao chaguliwa watashindwa kusafiri au wapatwe na shughuli mbali mbali basi wawili hao watawapa mafunzo zaidi katika shule yao ya hakuna mbrr entertainment.

Basi kama una hamu ya kuwa DJ, hakikisha unaskiza show hii bomba kila siku ya wiki kuanzia saa tisa hadi saa moja.

View Comments