Screenshot_from_2019_11_22_09_35_19__1574404591_63016

Jowie ambaye kwa sasa amezuiliwa kwa mwaka mmoja rumande ametoa ombi mpya kwa mahakama.

Joseph Irungu sasa anaomba aachiliwe kwa dhamana kama alivyopewa Jacque Maribe.

Maribe alipewa dhamana Oktoba 2018.

 Jowie ni mhusika mkuu katika mauaji tatanishi ya mfanyabiashara Monica Kimani.

Haya yanajiri huku babake marehemu Monica Kimani akisema bado anazongwa na fikra.

Kifo cha kutatanisha cha bintiye hadi leo kinamfanya kuwa na masimango akilini.

Paul Ngarama ambaye ni mhubiri amefunguka jinsi familia inapitia wakati mgumu.

Paul ameambia waumini wake wamwombee katika hali hii ngumu.

Kesi ya mauaji ya Monica bado inaendelea ili kubaini mahasidi waliomuua.

Mshukiwa huyu analalama kuwa anapata mahangaiko na tabu korokoroni.

"Ambaye tunatuhumiwa kosa moja na yeye (Jacque Maribe) alipewa dhamana na hajawahi susia vikao vya koti. Nahitaji hilo pia..." Alisema Jowie