magix

Mtayarishaji mkubwa wa muziki nchini Magix Enga ametangaza kumsamehe Harmonize staa kutoka Tanzania.

Akichapisha ujumbe kwenye Insta, Enga ametangaza kuwa sasa video na audio ya UNO inaonekana na YouTube.

Kuna uwezekano pande mbili zimepatana baada ya ubishi kuwepo kuhusu mdundo wa ngoma hiyo.

https://www.instagram.com/p/B5R91WHH25n/

"Tunaamini kuwa sanaa ya Afrika Mashariki ni kubwa kuliko sisi. Kwa sababu hii nimeamua kumsamehe Harmonize na nitairudisha UNO pale YouTube muda wowote..."

Siku chache nyuma, Meneja wa Harmonize alifunguka kupitia mtandao maridhawa wa Insta kuwa mdundo wa UNO ulifanana na Dundaing ya King Kaka.

“Tumepata taarifa kutoka mtandao wa YouTube kwamba producer wa Kenya ametuma baruapepe kudai umiliki wa ngoma ya UNO…”

https://www.instagram.com/p/B5Rk6v8Hoyy/

“Kwa utaratibu wa mtandao huu, ni lazima wafungie nyimbo hii kuonekana wakiendelea na juhudi za kufuata madai hayo…” alisema Mjerumani.

Ngoma ya Harmonize ilikuwa imefutwa YouTube kwa muda wa wiki tatu.