wanyama__1575116037_23539

Staa wa soka na ambaye ni kiungo wa kati wa Tottenham Victor Wanyama amenunua basi la abiria 40 ili kuzitunuku timu zilizomkuza ya Muthurwa Boxing Club na Country Bus FC

Mwanasoka huyu alikuwa anaichezea Muthurwa Boxing Club miaka ya awali.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, basi hili linatarajiwa kuandikwa nembo ya jina la klabu leo Jumamosi.

Aidha, basi hili lilifikishwa na kukaguliwa bandari ya Mombasa Novemba 29.

Hii hapa ni tuzo la basi lililonunuliwa na Wanyama.

Jopo lililoanzisha Victor Wanyama Foundation lilisema tuzo hilo litawamotisha wengi kupigania nafasi zao za kuwa mastaa wakubwa wa soka ,

“Tuna imani kubwa kuwa zawadi hii itatuwezesha kupata mastaa wengi wa soka katika Country Bus FC na Muthurwa Boxing Club,”

Akizungumza na gazeti la Daily Nation , Vicor alisema kuwa anafurahi kutunuku klabu kilichomlea.

“Siwezi kusahau kuwa nimezaliwa na kukulia Muthurwa na kuwa Country Bus FC ililea kipaji changu. Nafurahi kuwa nashukuru kwa kidogo nilichokipata na huu utakuwa mwanzo wa klabu hiki kupaa juu zaidi..." Victor Wanyama

View Comments