Screenshot_from_2019_12_02_09_57_38__1575269908_15368

Wikendi ilikuwa ya kunoga zaidi katika fiesta ya Karaoke katika sehemu ya burudani eneo la Kilimani.

Jacque Maribe alijiunga na marafiki waliofanya kazi pamoja katika runinga akiwemo Hassan Mugambi.

Matukio haya yote yalikuwa yanafanyika katika klabu ya Sands.

Hii huenda ikaashiria kuwa mwanadada huyu ameamua kujipa raha na kujisahaulisha na kesi zinazomwandama.

Maribe amekuwa akiandamwa na kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani.

Mwanadada huyu ameshtakiwa pamoja na Joseph Irungu katika kesi hii.

Aidha, wawili hawa walikanusha mashtaka dhidi yao.

Kulingana na jinsi kesi hii inavyoendeshwa, Joseph Irungu ndiye mshukiwa mkuu wa mauaji haya.

Jowie yupo katika rumande huku akiomba aachiliwe kwa dhamana kama Maribe.

Kesi ya Maribe itatajwa tena Machi 2020.

Mrembo huyu alijiachilia na kujipa burudani huku akiimba wimbo wa Aje wa Ali Kiba.

Tazama video hii:

https://www.instagram.com/p/B5jnqEsgTjw/

Hassan pia hakuachwa nyuma kuimba wimbo huo.

View Comments