Screenshot_from_2019_12_03_16_38_16__1575380328_30390

Hatimaye msanii wa kizazi kipya Akothee amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya tukio la kuanguka ghafla stejini.

Staa huyu wa kike alipatwa na kisunzi akiwa jukwaani Luo Festival iliyoandaliwa mji wa Kisumu.

Kwa mujibu wa meneja wake Nelly Oaks, mama huyu yupo katika hospitali huku hali yake ikichunguzwa na madaktari.

Tukio la kuzirai katika ukumbi wa burudani mjini Kisumu liliwashtua wengi.

Akothee anasema kuwa anashindwa na kulala nyakati za usiku.

" Nashindwa kulala usiku," Alisema akothee alipoulizwa kuhusu hali yake ya afya.

Akothee alianguka na kupoteza fahamu mwendo wa saa saba usiku wa Jumamosi.

Meneja wake aliriporitia tovuti ya Mpasho kuwa mkewe bado anapumzika.

"Akothee ana matumaini ya kupona hivi karibuni...' Alisema Nelly.

" Hata dawa za kuvuta usingizi hazisaidii kabisa. Nilikunywa mbili jana na nikakosa usingizi usiku wote...mwili umechoka sana..." Alisema Akothee.

View Comments