Jamaa aliyeomba kupatanishwa hii leo ni bwana Otieno, 29, akisema kuwa alikuwa mwizi na angependa kupatanishwa na babake, bwana Eli.

"Nilikuwa mwizi wa pickpocket huku nyumbani lakini niliwacha mwaka uliopita baada ya kuibia watu kwa mda mrefu." Alisema Otieno.

Aliongeza,

Baba ana chama nyingine na wakati huo sikuwa na kazi na yeye ndiye alikuwa anaweka zile fedha. Nilikuwa na hamu ya kuziiba lakini sijui alikoziweka kwani sikuziona hapo babangu akaleta shida na kusema hataki kuniona kwa boma lake baada ya kupata nimevunja mlango wake."

Otieno anadai alipata kazi ya kulisha ng'ombe lakini akaiba fedha na kuja Nairobi ambapo sasa amepata kazi.

Bwana Eli alipopigiwa simu alisema kuwa mwanawe aliwahi lala korokoroni kwa miezi miwili na akadai kuwa atabadilika, ila aliporudi alivunja mlango na kuiba mali nyingi.

Isitoshe akakimbilia Ahero na akaibia mama fulani na kupotelea Nairobi.

"Akiwa Nairobi akaanza kunitumia ujumbe mbovu mbovu na akadai amebadilika, hapo nikamwambia lazima twende kwa kituo cha polisi. Isitoshe tuite jamaa ambaye aliibia elfu thelathini na tumuombe msamaha kisha tujue jinsi tutamlipa."

Bwana Eli aliongeza kuwa mwanawe alikuwa na tabia ya kuiba kwa boma lake kwani ameoa wake watatu na alikuwa anawaibia wote. ALiongeza kuwa Otieno aliwahi muibia simu ya shilingi elfu 16 na kitita cha elfu tisa.

Hata hivyo, yuko tayari kumsamehe Otieno iwapo atarudi nyumbani na kuomba msamaha.

View Comments