- Raila Odinga
- Raila at DC grounds-compressed
- Raila with Musalia

Wafuasi na viongozi wa chama cha ODM walikuwa wamesisitiza kuwa kinara wao Raila Odinga aapishwe baada ya uchaguzi wa rais wa 2017 uliokumbwa na utata.

Katika wasifu wake, kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi anafichua kwamba kulikuwa na shinikizo kubwa kutoka wafuasi wao kuapishwa kwa Raila.

"Tuliambiwa kuwa jaji wa mahakama kuu na baadhi ya wanajeshi wako tayari kuja Uhuru Park na kumwapisha Raila Odinga kuwa rais. Hata ingawa sikujua jaji huyo au maafisa wao wa jeshi waliotazamiwa kuja," Mudavadi anafichua haya katika kitabu chake cha Soaring Above the Storms of Passion.

Mudavadi ambaye alikuwa mgombea mwenza wa Raila katika uchaguzi huo, anafichua zaidi kuwa alikuwa miongoni mwa waliopinga kuapishwa kwake kwa kuwa anasema ingetia taifa hili katika vurugu na vita.

Licha ya maandamano na vurugu, Rais Mwai Kibaki alikuwa ameapishwa tayari kwa muhula wa pili na Jaji Mkuu Evans Gicheru katika Ikulu ya Nairobi katika hafla iliyofanywa usiku wa manane.

Vita, rabsha na vurugu baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 ulisababisha zaidi ya vifo vya watu 1,300 huku maelfu yao wakivurushwa makwao.

Kitabu hicho cha wasifu chenye kurasa 417, kinapekua zaidi kuhusu mchakato wa kutuma matokeo ya uchaguzi ulikumbwa na itilafu katika Kenyatta International Conference Centre.

"Mgombeaji wetu na mimi tulitazama kila kitu katika Pentagon House. William Ruto, Andrew Ligale, Henry Kosgey na Caroli Omondi  ni watu wetu waliokuwa katika KICC. Tuliwatazama wakikabiliana na Kivuitu huku mambo yakizidi kuchacha," Musalia anasimulia.

"Siku ya tatu, tulienda kwa afisi za ECK katika KICC na kupata baadhi ya makamishina wakiwa tayari kumtangaza Mwai Kibaki kuwabingwa. Kulikuwa na hali ya taharuki. Martha Karua wa PNU alikuwa akiwasukuma sana kumtangaza," kinara wa ANC anasema.

Hata hivyo chama cha ODM kilisambaratika baada ya Musalia kubuni chama cha ANC 2012 na hata baadaye kutangamana tena na kubuni NASA katika uchaguzi mkuu wa 2017.

NASA ilidai kuwa uchaguzi huo wa 2017 ulikuwa wa kimapendeloa ambapo rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi katka chama cha Jubilee.

Kinyuma na ilivyo 2007 ambapo chama cha ODM hakikuwa na nia ya kuwasilisha kesi kortini kupinga matokeo ya uchaguzi, NASA waliwasilisha kesei mahakamani Agosti 2017.

Majaji sita wakiongozwa na Jaji Mkuu David Maraga walipuuzilia mbali uchaguzi huo kwa madai kuwa kulikuwa na mapendeleo na udanganyifu.

Na hata ilipotangazwa kurudiwa, Raila alijitoa kwenye kinyang'anyiro kwa madai kuwa tume ya IEBC haikuwa tayari kusimamia uchaguzi huo.

View Comments