Screenshot_from_2019_12_06_12_15_25__1575623945_74536

Mzazi mwenza wa Rayvanny, Fahyma amesema kuwa anamhurumia sana Nana.

Nana anahusishwa kutoka kimapenzi na Rayvanny.

Akihojiwa na Lilhommy TV, Fayhma amesema kuwa matatizo yake na baba mtoto hayachangiwi na Nana.

"Tena mimi namuonea huruma watu wanapomuunganisha na matatizo yetu.. Najua kilichotufanya tukosane," Alisema Fahyma.

Akihojiwa na Global TV publishers hapo awali, Fayma alisema kuwa wanaomhusisha Rayvanny na mimba ya Nana hawana akili.

“Mimi siwezi nikazungumzia chochote na huyo mdada kwa sababu amefanya tu wimbo na baba mtoto wangu lakini vitu zingine sizijui…” Fahyma.

 Mwanadada huyu aidha amesema Rayvanny amemfunza vitu vingi maishani.
"Amenifundisha vitu vingi sana. Ni mwanaume fulani hivi amenifunza maisha. Anajua jinsi ya kuishi na watu. Amenifanya nikawa mdada fulani ambaye najielewa sana..."
Fahyma amesisitiza kuwa ipo siku itafika aweke wazi tatizo linalowafanya wakosane.

"Sio huyo dada hahusiki kabisaa. Kwenye matatizo yangu na baba mtoto wangu hana makosa. Ipo siku nitaongea na kila mtu atajua..."