Iwapo unapanga kuandamana kesho  kwa ajili ya kukamatwa kwa gavana w anairobi Mike Sonko  ,basi umetahadharishwa na polisi. Msemaji wa polisi charles owino amesema yeyeote anayepanga kufanya maandamano anafaa kuhakikisha kwamba anatii sheria.

Gavana Sonko  amewahimiza wafuasi wake  kusalia watulivu na kuachana na mpango wa kwenda  katika mahakama ya milimani  atakapofikishwa hapo kesho. Wakili wake Harrison Kinyanjui amesema Sonko hataki malumbano yoyote kati ya wafuasi wake na polisi kwani ana uhakika atathibitisha kwamba hana hatia .

Masaibu ya gavana Mike sonko yameonekana kuzidi kwani polisi sasa wanasema wanalenga  kumshtaki kwa  kumshambulia afisa mammoja wa polisi wakati alipokuwa akikamatwa  huko Voi siku ya ijumaa. Charles Owino  amesema sonko pia atakabiliwa na mashtaka ya kuharibu vifaa vya wanahabari, kukataa kukamatwa na kuwauzia polisi kutekeleza kazi yao.

 

Hayo yakiarifiwa, wakili Harrison Kinyajui anasema  afisa wa polisi aliyenaswa katika video akimbeba juu kwa juu gavana wa Nairobi Mike Sonko wakati alipokuwa akikamatwa  anafaa kukamatwa .Kinyanjui anasema Sonko anahitaji huduma za dharura za matibabu kwani aliumizwa wakati wa tukio hilo .

 

Hayo yakijiri, watu 26  wangali hawajulikani waliko  na wanaminika kunaswa katika vifusi vya jengo liliporomoka mtaani Tassia siku ya ijumaa .maafisa wanaoendesha shughuli ya uokoaji wanasema idadi ya waliofariki bado ni watu watano  huku 33 wakiokolewa na 18 wamelazwa katika hospitali ya mama lucy .

View Comments