William Ruto na Duale wananitishia maisha, Mutua aripoti kituo cha polisi
Gavana wa kaunti ya Machakos Alfred Mutua ameandikisha taarifa katika kituo cha polisi kuwa naibu wa rais William Ruto na Aden Duale walimtishia maisha yake.
Mutua ameandikisha taarifa hizi katika kituo cha polisi Kilimani leo Jumatatu katika kitabu cha matukio na nambari 50/16/12/2019.
Katika kauli hiyo, Mutua aidha amemtaja seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen kama tishio kubwa kwa maisha yake.
Akihutubu nje ya kituo hicho cha polisi, Mutua amesema kuwa Duale na Murkomen walimtishia kumpiga vita kali ya kisiasa.
"Nilishambuliwa na mheshimiwa Duale na Murkomen kwa kuniambia ya kwamba ninawashambulia. Nilipowauliza eti ninawashambulia vipi wakasema eti nimekuwa nikimshambulia Ruto," Mutua amesema.
Mutua amesema kuwa Ruto aliongeza kumfokea 'wewe ngoja tu na utaona' mbele ya Duale ambaye pia alimwambia 'tulikukanya'