Diamond_Platnumz_bodyguard_shows_off_accident_wounds-min

Msanii wa kizazi kipya Diamond Platnumz amemzungumzia aliyekuwa mlinzi wake Mwarabu Fighter.

Haya yamejiri muda mrefu baada ya lebo ya WCB kumfuta kazi Mwarabu.

Baada ya kufutwa kazi katika sababu zisizoeleweka, Mwarabu katika mahojiano ya awalin alisema kuwa bosi wake alifahamu yote yaliyotokea.

https://www.instagram.com/p/B6PiIxfAy2T/

“Diamond Platnumz anaujua ukweli lakini pia Harmonize anaujua ukweli, wao wanatumia nyimbo zao kufikisha ujumbe lakini hawataki kuongea ukweli.

"Mi nafurahi wanavyoniongelea kwani bado wanakumbuka makubwa niliyowafanyia” alisema Mwarabu.

https://www.instagram.com/p/B6Q7zDDpChn/

Katika posti la Insta la kuwakaribisha wasanii wakubwa Tanzania katika tamasha la kufunga mwaka mjini Kigoma, Mondi amemkaribisha Mwarabu na kuchora ujumbe huu.

" Amini kwamba Diamond Platnumz alijengwa na anajengwa na watu wengi ambao usiku na mchana wanapambana kuhakikisha kwa pamoja na kijana wao tunafikisha sanaa yetu Mbali... My brother  KIGOMA inakusubiri ikupe Shukran za Dhati...."

Posti ya staa huyu inaonyesha kuwa hakuna bifu iliyopo kati yake na Mwarabu Fighter ata kama alimpiga kalamu.