Ni takriban miezi minne tangia msanii Kambua ajifungue mtoto wa kiume, na kila siku amekuwa akiimba nyimbo za kumsifu mungu wa Sarah ambaye baada ya miaka mingi bila kujaliwa na mwana, alimkumbuka.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Kambua amekuwa akipeana ushuhuda wake wa jinsi alivyomngoja mola baada ya wengi kumsengenya kwa kukosa mwana.

Hatimaye alipotangaza kuwa anatarajia mtoto, dunia mzima ilisimama na kusherehekea miujiza ya mola. Wasanii wenza wakenya kutoka tabaka mbali mbali walifurika katika mitandao ya kijamii na kumnyunyuzia jumbe za furaha na hongera.

Msanii huyo ambaye ameolewa na mchungaji Jackson Mathu, hivi majuzi alifunguka kuhusu safari yake ya mimba na mwishowe ilivyombidi ajifungue kupitia upasuaji.

Alisema,

“This is me thanking God that I can fit into one of my pre-preggers dresses. My body has changed alot and I am embracing it all. I stretched in ways I never knew were possible! Isn’t God amazing? And then went through a CS (story for another day). Recovering from it is not a joke!” she wrote on Instagram.

Alisema kuwa kwa sasa kazi kuu ni kujichunga na kumlea mwanawe kwa namna bora huku akisema kuwa licha ya mwili wake kubadilika kwa kiwango kikuu, anamshukuru mola kwa kumfanya mzazi na hajutii lolote.

Hii leo amefunguka kuhusu jinsi watu walimuita majina na kumkejeli kuwa hana uwezo wa kubeba mtoto. Isitoshe, watu hao hao walimwambia kuwa hawezi keti nao na walimnyamazisha kila walipopata fursa.

Aliandika,

All it takes is one move from God. Just one, and your story changes. They called me all sorts of things! Constantly reminded me that I didn't have a seat at the table. Silenced me at every opportunity. But in the wait, and the longing, God looked at me and said I was worthy. He saw me as complete, lacking nothing. He reminded me that He is the God who changes times and seasons.

Hata hivyo, aliendelea na ujumbe wake huku akimshukuru mungu kwa kupanguza machozi yake na kumfanya mama.

And after all the noise, after the mockery and public shaming, Jehovah Himself arose! He wiped my tears and gave me a new name. I am a mother y'all! To the cutest little boy I have ever laid my eyes on. This covenant-keeping God is only getting started with me, and I am not running after miracles; I'm running after His heart. 💛

https://www.instagram.com/p/B6Qf_J1gi4M/