Wavuvi 8 ambao mashua yao ilizama majini huko Ziwayu, Kaunti ya Kilifi, wamepatikana wakiwa hai. Wote wako katika hali mahututi na wanapokea huduma maalum ya matibabu kwa sasa katika hospitali ya Malindi.

Walipatikana katika bahari na wavuvi wengine, wakiwa wamesombwa na maji umbali wa masaa saba kutoka eneo mashua yao yalizamia.

Mkusanyiko wa habari;

Unaposherehekea msimu wa krismasi hakikisha umetenga pesa utakazotumia mwezi wa Januari. Mtaalam wa masuala ya kifedha Sammy Ndirangu akushauri kutotumia fedha zako kwa matumizi ambayo hukuyapangia.

Kama wewe na mme ama mke wako mmelazimika kuisha katika maeneo tofauti kwa sababu za kikazi, mnashauriwa kuhakikisha mnaonana mara kwa mara. Huyu hapa mwanasaikolojia Moffat Kago na mengi.

Je, wewe huzua vurugu ya maneno, ya kihisia au ya kimwili wakati wowote unapohisi kutishiwa katika uhusiano wako unahitaji kutafuta msaada. Mtaalma wa uhusiano James Mbugua anaeleza

Watu waili walifariki papo hapo baada ya gari lao kuligonga gari la mafuta katika barabara ya Southern bypass eneo la Lang'ata. Kamanda wa Lang'ata Gregory Mutiso anasema huenda vijana hao wawili walikuwa wakiliendesha gari lao kwa mwendo wa kasi sana wakati wa ajali hiyo.

Maafisa wa upelelezi aktika kaunti ya Migori, huko Suna Mashariki wanamtafuta mwanamke mwenye umri wa makamo ambaye alitoweka baada ya kumdunga kisu shemeji yake. Inaaminika Eunice Adhiambo alimdunga kisu mwanamme huyo baada kuzozana.

Mkusanyiko wa habari za spoti;

Barcelona itajaribu kumsaini mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 27, katika dirisha dogo la mwezi Januari.

Chelsea inafikiria uhamisho wa mwezi Januari wa mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 23.

Kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba, 26, anataka kuondoka katika klabu hiyo na kurudi katika klabu yake ya zamani Juventus.

Mario Mandzukic amemaliza uvumi uliokuwa ukienea baada ya kukamilisha uhamisho wake katika klabu ya Qatari ya Al-Duhail licha ya Man United kuonyesha hamu ya kumsajili kutoka Manchester United.

View Comments