Screenshot_from_2019_12_28_12_29_43__1577525415_65759

Video ya mcheshi Eric Omondi akipiga densi moja hatari na msanii wa muziki wa kizazi kipya Akothee imezua gumzo katika mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo fupi iliyosambaa kwa kasi Insta, Eric anaonekana katikati mwa mabinti wengi wakijipa raha katika sehemu ya burudani.

Mwanamitindo Vera Sidika hajaachwa nyuma katika sherehe hizo za kufunga mwaka wa 2019.

Tazama hapa:

https://www.instagram.com/p/B6kcIVMlQEe/

Densi hiyo ilifanyika mkesha wa sikukuu ya krismasi huku mastaa wengi nchini wakionekana katika video hiyo.

Omondi anaonekana kufurahia tukio nzima huku akipata nafasi adimu sana ya kusowera na mwanamitindo Vera Sidika.

Msimu huu wa krismasi na mwaka mpya huwa umesheheni burudani za kila aina na hii ilikuwa moja ya kupigiwa mfano.

View Comments