Kwa kweli mapenzi ni kihozi na hayafichiki na wapendanao hufanya kila namna kuhakikisha kuwa mapenzi yao yanadumu na wanafurahishana.

Hata hivyo, kuna mahali mambo hufika na mapenzi yanaisha, madharau yanaingilia ndoa na hivo ndivyo ndoa husambaratika.

Mwanamke mmoja kwa jina Lucy, aliwashangaza waskizaji alisimulia jinsi mume wake alivyomletea watoto wanne kutoka ndoa ya zamani na kumtenga pindi tu walipojaliwa watoto wawili pamoja.

Kulingana na Lucy, alipatana na mumewe wakati alikuwa hohe hahe na wawili wakavumiliana bila yeye kujali kuwa analea watoto wa mke wake wa kwanza. Hata hivyo, wawili walijaliwa na mali na hapo ndipo bwanake alianza kujionesha ngozi yake kamili.

Jamaa aliwacha kushughulikia familia yake, na ilimbidi Lucy kuanza kufanya vibarau kadhaa wa kadhaa ili awashughulikie watoto sita. Kuzidisha, bwanake alienda nje na kupachika mke mwingine mimba na wakapata watoto mapacha.

Bila heshima aliileta ile familia kwake jambo lililomkera Lucy na kumpelekea kutaka kujitoa uhai kwa kunywa sumu.

Soma usimulizi wake.

Massawe mimi nikiolewa nilipata bwana yangu ameoa bibi wa kwanza ameenda amewacha watoto wanne, nikiolewa na yeye alikuwa mtu wa kuchunga ng'ombe.

Nimehangaika na watoto nimefanya vibarau kwa mashamba ya watu, nimeenda forest nikitoa kuni nikiuza kusudi hawa watoto wapate chakula.

Bwanangu ilikuwa Jumapili  ameniletea mwanamke na watoto wawili, Massawe jambo hilo limeniuma. Kando ya hao watoto wanne, ameoa, amepatia mwanamke mimba na amezaa mapacha wawili. Nashukuru mungu kwa sababu maisha yenye nimepitia ni mungu tu anajua hata ilifika mahali nikanywa sumu kwani moyo wangu unaniuma zaidi.

Tumezungumza na mume wangu na akasema mtu akitaka kujiua ajiua mtu akitaka kwenda aende kwani hana shughuli.

Bwanangu alileta watoto kunyoa kisha akarudi nao na akaniwachia wanne pamoja na wawili tulioa naye. Mmoja wa miezi sita na mwingine wa mwezi mmoja. Napanga mungu akinifungulia mlango kidogo nijiondee kwani dalili ya mvua ni mawingu.

Kinachomuudhi Lucy ni kuwa baba mkwe ndiye anayeingilia ndoa yake na hana mtu yeyote wa kuendea kila anapotaka kutatua shida za ndoa yake.

Aliongeza: Kitu kinachoniuma ni eti bwanangu hana wazazi kwani wote waliaga na mwenye alibaki ni babake mdogo na ndiye kunipangia hayo yote, imeniuma sana. Baba mkwe ameingia kwa ndoa yangu kwa kichwa na miguu.

&feature=youtu.be