guest.000

Leo katika kitengo cha ilikuaje, alyekuwa mgeni wetu ni bi Janet Muva anayetambulika kama Membu Chenge, katika mitandao ya kijamii.

Bi Chenge ambaye amejaliwa wana watatu, ni mtaalamu wa mambo ya ndoa na mahusiano na amerudi nchini baada ya kuishi Ujerumani kwa miaka kumi na mitano.

Alipoulizwa kuhusu ndoa za kisasa na sababu zao kubunjika alisema;

"Sisi binadamu wengi tunakimbilia ndoa na inataka mtu mjinga kumaanisha uwe muombaji msamaha na mvumilivu" Alisema kuwa ameolewa kwa miaka 23.

Siri ya ndoa?

"Nimekuwa zuzu katika ndoa nimepanda milima na mabonde. Maisha ya uchumba hayana ukweli na kwa ndoa unakutana na ukweli kwani baby yule ukiolewa ni wachache sana huendeleza yale yale mambo."

Membu alisema kuwa ndoa sio rahisi na imembidi kuwa mstahimilivu na mjinga mara kwa mara ili ndoa yake isisambaratike.

Mume wangu ni mbinafsi sana na yeye husema kuwa napenda kuzungumza sana 

Wanandoa wanafaa kuwachana na miaka mitatu au mitano kwa sababu msichana akiolewa na mzee ikifika ni tendo la ndoa kwani mlingoti hausimami.

Aliongeza akisema kuwa heri apate raha ya kitandani au kurusha roho ama ukipenda raha ya dunia kuliko kupata jamaa mzee mwenye mali ambaye hatamridhisha.

Alipoulizwa kuhusu utofauti wa mapenzi na ndoa vya wa Afrika na wazungu alisema;

Mapenzi ya muafrika magani? Mzungu anaweza kuoa ili tu akakupige mabusu na ni hivyo, mapenzi ni kati ya wazungu na wazungu ila mzungu na muafrika ni hela tu.

Ushauri wake kwa wakenya ni kuwa wasiogope ndoa akisema kuwa mwanaume anataka kutunzwa na anataka kudekezwa kama tu mtoto.

Kwa wanaume;

Unapomuoa mtoto wa mtu mlee na mtunze kwani utazunguka ma butchery na nyama ni ile ile.

View Comments