- HARRY AND MEGHAN
- Malkia Elizabeth

Harry  na Meghan  wameamua kujiondoa kutoka familia ya kifalme nchini uingereza lakini uamuzi huo utakuwa mzito kwao .Wasaidizi na maafisa wa Kasri  la Buckingaham hawajafurahishwa na hatua hiyo  kwani wanasema licha ya familia ya kifalme kufanya kila jambo kukubali uhusiano kati yao tangu mwaka wa 2016 ,wanandoa hao waasi wameamua kuondoka familia ya kifalme  bila kushauriana na Malkia , Prince Charles  na Prince William.  Uamuzi  wao kwamba wanataka kuishi  marekani kaskazini na Uingereza  ulifanywa bila ufahamu wa familia yao  na wengi walipata kujua kinachofanyika katika vyombo vya habari jana usiku .

Wanandoa hao wametangaza hilo  wiki sita tu baada ya kurejea kutoka safarini Canada  walipokuwa katika mapumziko na hatua ya kujiondoa kutoka majukumu ya kifalme imeonekana kama jambo kubwa na ambalo hakuna aliyewahi kufikiria linaweza kutokea . Wandani wanaotetea kuwepo kwa familia ya kifalme na mfumo wake wa maisha wameshangaa mbona Harry na Meghan waliopewa kila kitu ,Harusi waliotaka,nyumba waliotaka ,pesa na safari za nje ya Uingereza walivyoamua ghafla bila kumshauri yeyote kuondoka familia ya kifalme .

Harry na Meghan  hata hivyo wamesema wako tayari kuendelea kumsaidia Malkia katika majukumu yake ya kifalme na pia kuanza mkondo mpya wa maisha yao ili kupata uhuru wa kifedha na kumlea mwanao katika mazingira ya ukuuzi wa kifalme . Katika taarifa iliyotolewa na Kasri ya Buckingham  imesema -  ‘Mazungumzo kati ya Duke na Duchess wa Sussex  yapo katika hatua za mwanzo . tunaeleewa ari yao ya kutaka kuchukua mkondo tofauti  ,lakini masuala haya ni mazito  na itachukuamuda kuyajadili’.‘Usiri mkubwa uliozingira  uamuzi wa wawili hao ni kama kisu kilichowachoma kabisa watu wote wa familia ya kifalme.Ni kama usaliti mkubwa sana’ mndano mmoja wa  Kasri amenukuliwa akisema .

View Comments