Renson, 23, aliomba apatanishwe na Cynthia, 19, akidai walikosania kitu kidogo na saa hii hataki maneno yake.

Wawili hao wamekuwa kwa uhusiano wa miezi kumi na moja.

"Sijui nini kilitokea kwani nilipotoka nyumbani kila kitu kilikuwa sawa lakini kenye nakumbuka nilimwambia asiende klabuni kwani kila akienda ana vituko. Hapo sijui ni kama alidhani namkazia maisha na kutoka hapo akadai hataki maneno yangu na sikuelewa." Alieleza.

Aliongeza,

Siku moja nikakutana na aliyekuwa mpenzi wangu na tukapiga picha ambazo mpenzi wangu aliona na akanizushia sana." 

Anadai kuwa mara nyingine tena yule msichana alitokea tena mahala Renson yupo kwa swimming pool na mpenziwe akadhani wana uhusiano.

Alipopigiwa simu, bi Cynthia alidai kuwa amechoka kwani alikuwa hepi jana usiku na amelala. Licha ya hilo alisema kuwa ameskiza Renson na amemsamehe.

"Hata kama ni coincidence haiwezi kuwa mnapatikana kila wakati. Namtakia mema aweze kunufaika na yote anayofanya maishani ila sijui kama nampenda." Alisema Cynthia.

Hata hivyo, Renson alirithishwa na hilo kwani anakiri hawezi lazimisha mapenzi.

View Comments