CRIMINAL or VICTIM? Ufichuzi watolewa kuhusu mwalimu aliyeuawa na mwili wake kuchomwa Kitui .
Mauji ya Mwalimu wa Kiswahili na hesabu Daisy Mbathe Mbaluka yaliishangaza nchi nzima siku ya jumatatu huko Kitui . Mwanzoni ilidaiwa kwamba mauaji yake yalitokana na matokeo mabaya katika shule ya msingi ya Ndooni lakini sasa uchunguzi uliofanywa na polisi umetoa tasira tofauti sana ya hali halisi .
Inadaiwa marehemu alikuwa mwanachama wa genge la wahalifu ambao wamekuwa wakiwahangaisha wakaazi wa eneo hilo . Mbathe ,imeripotiwa alikuwa akitumia urembo wake kuwahadaa wanaume katika nyumbani kwake ,kisha baadaye wanachama wengine wa genge lake kuja na kuwavamia waathiriwa na kuwalazimisha kutoa pesa . wakaazi wa eneo hilo wamesema msururu wa mahangaiko ambayo amewasababishia watu wengi ulimfanya kuwa lengo kwa wenyeji waliotaka kumwua . Inadaiwa wanakijiji wengi walifahamu kwamba mwalimu Mbathe angeuawa lakini hawakajua ni lini kuagamizwa kwake kungetekelezwa .
Katika masoko ya makuka na malalani huko Kitu mashariki ,wakaazi wanajadili mauaji ya Mbathe ,lakini hakuna anayetaka kusikika .wengi wanaonekana kuridhishwa na mauaji hayo .Polisi wanasema maandamano ya wazazi kulalamikia matokeo mabaya ya shule ya ndooni ,yalitumiwa kumvizia mwalimu huyo aliyekuwa akiwapeleka binti zake wawili shuleni .waliotekeleza mauaji yake walimkatakata kwa panga kabla ya kuuchoma mwili wake huku wanawe wakitorokea usalama wao katika maboma yalio karibu . Polisi wanawasaka washukiwa waliohusika na mauji ya mwalimu huyo na tayari wawili wamefikishwa kortini kuhusiana na mauaji hayo.