SAD:Mvulana mwenye umri wa miaka 11 amuua kakake wakipigania chaja ya simu
Mvulana amwenye umri wa miaka 11 aliyemuua kakake kwa kumdunga kisu wakipigania chaja ya simu atazuiliwa katika rumande ya watoto kwa siku tatu ,mahakama ya Nakuru imeagiza. Upande wa mashtaka umetaka kupewa muda kushauriana iwapo mwanafunzi huyo wa darasa la tano anafaa kushtakiwa .
Polisi wanashikilia kwamba mtoto huyo lazima ashtakiwe lakini mawakili wake wanasema kesi hiyo inafaa kutupiliwa mbali kwa msingi kwamba hawezi kushtakiwa kwa sababu ya umri wake mdogo . Wakili wake anasema kwa mujibu wa sheria mtu aliye chini ya umri wa miaka 12 hana uwezo wa kutekeleza uhalifu givyo basi mtoto hakujua iwapo ni hatia kumwua kakake .
Mtoto huyo atazuiliwa katika rumande ya Nakuru Children’s Home huku mahakama ikingoja ripoti ya kuamua hatua itakayofuata . Mtoto huyo anadaiwa kumuua kakake mwenye umri wa miaka 15 disemba tarehe 31 mwaka jana katika viunga vya mji wa Nakuru .Wawili hao walianza kulumbana wakati mshukiwa alipoitoa chaja kutoka kwa rununu ya kakake . majirani wanasema wazazi wao walikuwa wamesafiri mashambani kwa sherehe za krisimasi na kuwaacha watoto hao chini ya utunzi wa mjomba yao.mahakama itatoa uamuzi wa iwapo itamshtaki mvulana huyo januari tarehe 16 mwaka huu .