emma Too

Sio kila siku unajipata ukiwa umeorodheshwa miongoni mwa watu warembo zaidi duniani, na kwa kweli sio jambo ndogo au la kudharauliwa.

Hata hivyo, mrembo kutoka humu nchini, Emma Too aliwahi orodheshwa kama mmoja wa watu warembo zaidi mno duniani na jarida la People Magazine mnamo mwaka wa 2006.

Leo ikiwa siku ya alhamisi, Emma alichukua fursa hiyo kuwakumbusha wanawake duniani kuwa rangi nyeusi kwa kweli yang'aa.

Kupitia mtandao wa Twitter aliandika,

MY DARK-SKINNED SELF MADE IT ON 100 MOST BEAUTIFUL PEOPLE IN THE WORLD BY @PEOPLE MAGAZINE. LATELY, I HAVE BEEN READING A LOT ABOUT YOUNG WOMEN WHO HAVE INSECURITIES ABOUT THEIR DARK SKIN, PLEASE LET NO ONE TELL YOU WHO & HOW YOU SHOULD BE, BLACK IS BEAUTIFUL, LOVE YOUR SKIN.”