HELP! I NEED A HUSBAND: Mrembo ambaye amekuwa na uhusiano na wanaume 21 lakini hakuna aliyemwuoa .
Hakuna kinachotisha kama kupata na fikra kwamba mpenzi wake wa dhati siku moaja naweza kukuacha ghafla bila kukupa sababu tosa . Watu wengi kabla ya kutimu umri wa kutaka kuoa au kuolewa huwa na idadi Fulani ya wapenzi wa zamani yaani ‘exes’.Lakini hujawai kupatwa au kusikia masaibu anayopitia Jane Kiiru ambaye amewahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi sio mara moja au mbili au tatu…bali mara 21 na wanaume tofauti ambao alikuwa amejua wangefunga ndoa lakini maisha yake yamekuwa ya kufadhaishwa na kila mmoja wao .Hiki ni kisa cha mwanamke mwneye umri wa miaka 35 ambaye sasa amejitokeza wazi kusimulia anayopitia na ashauriwe kuhusu makosa yake ambayo labda yanamfanya kutoweza kufaulu kupata mwanamme wa kumwooa .
Tangia alipokuwa kidato cha kwanza hadi alipomaliza shule ya upili ,Jane amekuwa na wapenzi sita katika nyakati tofauti . Anasema amekuwa akifanya uhusiano na wanaume na wanapotengana anapata ugumu wa kusalia ‘single’ na hivyo basi anajipata katika mikono ya mwanamme mwingine .Tatiz ni kwamba wanaompokea mara ya kwanza kumwonea huruma anapowasimulia masaibu yake lakini baada ya kipindi Fulani wao pia humwacha.Je,tatizo ni jipi? Mtu anafaa kuwa na wapenzi wangapi kabla ya kumpata Yule watakayedumu naye?
‘Tatizo langu ni kwamba singeweza kungoja kwa muda kabla ya kuanza uhusiano mwingine ,naogopa kuwa lonely’ Anasema Jane . Ila masaibu yake haya yamenifanya nifanye utafiti kidogo kuhusu suala hilo,Je ni wapenzi wangapi unaofaa kuwa nao kabla ya kumpata Yule Mmoja? How many frogs should you kiss? Jane anasema baadhi ya uhusiano wake ulikuwa ukitamatika hata baada ya miezi miwili. ‘Ningeweza kukutana na mwanamme kasha anipendeze mwanzoni ,after a few days, najipata tu ameanza kunibore’. Anasema Jane .
Mtu anafaa kuwa na ex wangapi kabla ya kumpata mpenzi wa kuingia naye katika ndoa?Kupata jibu la swali hili ni kibarua ambacho sasa nimechoka kufanya .Kila mwana dada unayemuuliza anakupa jibu la kuzungusha lakini waliojaribu ni wachache. Matokeo ni kama ifuatavyo lakini najua wengi ndani ya nyoyo zenu mnajua jibu .Mhusika wa kwanza Nancy* amesema anaweza kuwakumbuka wapenzi watano wa zamani kabla ya kukutana na mume wake .Jeptoo* amesitasita kwa zaidi ya dakika tano lakini anasema ni takriban wanaume sita au saba.Esther* amesema aliopitia yanazua kumbukumbu za machungu sasa hawezi kutaka hata kuwahesabu ilhali Stella ,amenifanyia mzaha kwa niambia 'Leta calculator na ukae chini ungoje jibu'. Bado nacheka . Kama kuna siri kali ambayo wanawake wataiweka katika nyoyo zao licha ya makali ya ndimi zao ni idadi kamili na halisi ya wapenzi wa zamani .Kama mwanamme usitake kupata jibu lakini kuna waliobahatika kwa kumpata mmoja aliyesalia kuwa NDIYE!