PATIKANA: Bastola aliyotumia Babu Owino kumpiga risasi DJ Yapatikana
Bastola ya mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ndio iliyotumiwa katika kisa cha ufyatulianaji risasi na kusababisha kujeruhiwa kwa mtu mmoja katika eneo la burudani la B Club ,Polisi wamesema . Mkuu wa polisi wa Kilimani Lucas Ogara amethibitisha hilo akisema mwathiriwa yupo katika hali thabiti . “ Hatuwezi kutaja jina la mwathiriwa kwa sababu ni kinyume cha sheria . lakini tumepokea ripoti kwamba risasi ilipitia shingoni mwake’. Ogara amesema .
Ogara amesema wanamzuilia Owino katika kituo hicho nab ado hajaandikisha taarifa .DCI imesema imapata risasi tisa na ganda moja la risasi katika eneo la tukio ."... Vyote vimewekwa kama ushahidi na vitachunguzwa na watalaam wa bunduki’ mkurugenzi wa DCI George Kinoti amesema .
https://twitter.com/DCI_Kenya/status/1218112033025077250?ref_src=twsrc%5Etfw%7Ctwcamp%5Etweetembed%7Ctwterm%5E1218112033025077250&ref_url=https%3A%2F%2Fwww.the-star.co.ke%2Fnews%2F2020-01-17-babu-owinos-gun-used-in-kilimani-shooting-police%2F
Awali wakili wa Babu Cliff Ombeta amesema mteja wake alikaribiwa kwa njia ya kimabavu na mtu aliyemdhani kuwa rafiki yake na kusababisha purukushani . Amethibitisha kwamba bunduki ya Babu sasa imechukuliwa na polisi na mbunge huyo ana leseni yakuwa na bunduki . Wakili wake amesema tukio hilo sio la mauaji kwani mwathiriwa yungali anapokea matibabu hospitalini .