BATTLE FRONT :Jinsi Hatma ya Waititu inavyozua vita vya ndani kati Uhuru na Ruto .
Washirika wa rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wapo katika vita vya chini kwa chini kuhusiana na kura ya kumwondoa afisini gavana wa Kiambu Ferdinad Waititu ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi . Rais Kenyatta inaripotiwa anataka Waititu aondolewe uongozini ili kuafikiana na uamuzi wa waakilishi wa kuanti ya Kiambu na wakaazi ambao wamekuwa wakilalamika kuhusu utendakazi wake na kukithiri kwa ufisadi . Naibu wa rais kwa upande wake analenga kumsaidia Waititu kuepuka kibaridi cha kusalia nje ya maamlaka hasa kwa ajili ya umuhimu wake katika kumsaidia Ruto wakati wa kampeini za kumritihi rais Kenyatta mwaka wa 2022 .
Waituti, mkewe Susan wangari na wengine wanane wanakabiliwa na mashtaka ya ufisadi kuhusiana na kandarasi zenye thamani ya shilingi milioni 580 ambazozilitolewa kwa kampuni zinazodaiwa kutoa hongo . Waakilishi wa kaunti ya kiambu walimwondoa waittu afisini mwezi uliopita na sasa senate inangoja kufanya kikao siku ya jumanne ili kuamua hatma yake .
Tangu mwaka wa 2013 senate imeidhinisha tu kuondolewa maamlakani kwa gavana mmoja . Duru zaarifu kwamba maseneta wanaomwunga mkono rais Kenyatta wanashirikiana na maafisa wenye ushawishi mkubwa katika ikulu ,ili kuhakikisha kwamba uamuzi wa walkilishi wa kaunti ya Kiambu wa kumfurusha Waititu afisini unatekelezwa . Waititu mwenyewe amepinga vikali kuondolewa kwake akidai kwamba bunge la kaunti halikuwa na idadi inayohitajika ya waakilishi wa kaunti kuufanya uamuzi huo .