PATANISHO: Shiro anataka kumrudia Kamau ‘Mruka mimba’.
Leo katika patanisho Shiro kutoka Nakuru aliye na umri wa miaka 34 ametuma ujumbe akitaka kupatanishwa na mpenzi wake Kamau ambaye ana umri wa miaka 31. Shiro amesema anataka tu kurudiana na Kamau licha ya kwamba amekataa kukubali mtoto ambaye wamezaa naye .Hii ni baada ya Kamau kuikataa mimba ya Shiro akisema siye baba ya mtoto lakini ushahidi na kila maumbile ya mtoto huyo wa kike yanafanana na Kamau . Shiro amesema ‘ Sitaki alee mtoto,nina pesa zangu za kulea mtoto’.
Kamau alipopigiwa simu amesitasita na hataki kuzungumza na shiro kwa sababu anadai alimtukana .
Kamau amedai kwamba Shiro alimtukana kwa kumwita ‘kihi’. Katika lugha ya kikuyu ,mtu anayeiitwa ‘Kihi’ ni Yule ambaye hajatahariwa .
Lakini Shiro yuko tayari kulipia vipimo vya DNA ili kuthibitisha kwamba mtoto huyo ni wa Kamau . Wawili hao wana mengi ambayo yamewatenganisha na mengi yalifichuka wakati Shiro akizungumza na Gidi na Ghost baada ya kusema pia kwamba Kamau alikuwa na mke na walikutana wakati mke wa Kamau hakuwepo .
Jitihada za Gidi kumshawishi Kamau akubali kumsamehe Shiro ili warudiane ziligonga mwamba wakati Kamau alipokata simu kwa mara ya pili lakini mpenzi wake Shiro anasema labda ni kwa sababu mke wake yuko karibu naye . Akihojiwa mbona ametaka sana kurudiana na mume wa mtu ,Shiro amecheka akisema ‘Ni mzuri tu lakini ameharibiwa na wanawake wa facebook’. Ameongeza kusema ‘Hata Kamau aliniblock facebook ati nina rafiki wengi na atapatwa na ulcers’.
Kingine ambacho Shiro anahisi kimewatenganisha ni uchochezi wa baadhi ya rafiki zake wa kike ambao walimahamisha Kamau kwamba Shiro alikuwa ameolewa huko Thika .Hilo limeonekana kumkwaza sana Kamau ambaye yamkini ameshafanya uamuzi wa kutoendelea na uhusiano huo .Alipoulizwa na Gidi iwapo hamtaki tena Shiro,Kamau alisema
‘ Sitaki Mambo mengi….Simtaki’
Kamau ana umri mdogo kumliko Shiro na hilo pia huenda likawa mojawpao ya sababu zinazoyumbisha uhusiano wao .
Shiro hata hivyo amesimama kidete akisema lazima atamrudia Kamau akisema ‘Sitamwacha hivyo,Nampenda’. Ameahidi kumpigia simu baadaye ili kumshawishi warudiane .Je,mapenzi yao yataweza kuokolewa?