nYAKUNDI

 Makachero wamemkamata mwanablogu Cyprian Nyakundi na mshukiwa mwingine  Emmanuel Nyamweya Ong'era  kwa njama ya kutaka kupokea shilingi milioni 17   ili kuondoa chapisho la mtandaoni la kumharibia mtu jina .

Wawili hao tayari walikuwa wameshapokea shilingi milioni 1 kama sehemu ya malipo hayo .

https://twitter.com/DCI_Kenya/status/1219238606184894464

Inadaiwa wawili hao waliitisha kiasi hicho cha pesa kama  sharti la kuondoa chapisho hilo kutoka kwa blogu inayomilikiwa na Nyakundi . wawili hao watazuiliwa na polisi hadi Jumanne tarehe 21 watakapofikishwa kortini . Pesa hizo pia zilipatikana  na zitatumiwa kama ushahidi .

View Comments