HELL:Wakili wa Miguna Miguna asema mteja wake anapitia mateso Ulaya
Jitihada za Wakili Miguna Miguna kurejea nchini zimepatwa na pigo jingine baada ya mahakama kuahirisha kesi yake hadi machi tarehe 23 machi . Wakili wake John Khaminwa amefichua kwamba mteja wake anaipitia mahangaiko barani ulaya .Khaminwa alikuwa akijibu hatua ya mahakama kuisongesha kesi yake hadi Machi bila yeye kuwepo .
Ameshtumu wakili kutoka afisi ya mkuu wa sheria kumruhusu hakimu kuisikiza kesi hiyo saa tatu asubuhi ,saa mbili mapema kuliko muda ambao kesi hiyo ilifaa kusikizwa saa tani asubuhi kabla hajafika kortini .Khamninwa amesema atawasilisha kesi kortini kupinga kusongeshwa kwa kesi hiyo hadi tarehe 23 machi anayosema ni mbali sana . Wakili wa tume ya kitaifa ya kutetea haki haki za binadamu Victor Kamau alikuwa kortini wakati uamuzi huo ilipotolewa .
Jaji wa mahakama kuu John Mativo alikuwa amemwagiza mwanasheria mkuu Kihara Kariuki kutoa maoni ya ushauri kueleza mbona aserikali ilikuwa imekiuka agizo la kufanikisha kurejea nchini kwa Miguna . Kihara alimtuma mwakilishi kortini lakini mawakili wa Miguna walimkataa wakisema suala hilo lilifaa kushughulikiwa na mkuu wa sheria mwenyewe . katika uamuzi wake jaji Mativo alisema mwanasheria mkuu kama ‘rafiki’ wa mahakama alifaa kutoa maelezo kuhusu hatua ya serikali kukataa kufanikisha kurejea nchini kwa Miguna .