Maid 1

Mfanyikazi mmoja wa nyumbani mwenye umri wa miaka 51 huko Mombasa amelazimika kuacha kazi yake baada ya bosi wake kuanza kumtaka afanye vitendo vya kushangaza.

Chidzuga Mwangoka ( sio jina lake halisi )  aliacha kazi yake Novmba mwaka jana  baada ya kumafnyia bosi wake kwa zaidi ya miaka 10  kwa  ajili ya malipo duni, kazi nyingi na muda mrefu wa kufanya kazi .

Hata hivyo baada ya mwezi mmoja, bosi wake  ambaye ana biashara ya utengezaji wa vitambaa vya nguo alimpigia simu na kumtaka arejee kumfanyia kazi kwa ahadi ya kuteeleza kila alichokitaka.

“ Nilikubali kurejea kumfanyia kazi," amesema Mwangoka.

Lakini Mwangoka anasema bosi wake alianza kumtaka amfanyie vitu vya kushangaza  kama vile kumkanda . “ Mwanzoni, nilifikiri maombi yake haya hayakuwa na hila kwa sababu angelalama kuhusu maumivu ya misuli  na uchovu’ Mwangoka amesimulia .

Alianza kumkanda bosi miguu, mikono na mgongo.

“ Hata hivyo alianza kunitaka  nimkande mapajani na nikaanza kupata ugumu kidogo’ Bosi naye akawa mkarimu na hata akampa zawadi ya Friji na runinga ya inchi 42. “ Nilifikiri kuacha kazi kulimfanya agundue  kwamba alihitaji msaidizi katika jumba lake kubwa alimoishi na mkewe wa tatu’.

Mfanyibiashara huyo anayeishi katika mtaa wa kifahari wa kizingo  ana watoto wanne aliowapata katika ndoa zake mbili za hapo awali.  Wake zake  wawili wa zamani walifariki na wanawe wanne wanaishi Uingereza .

Mwanamume huyo hana mtoto na mkewe wa tatu. Kuelekea mwezi Disemba mwaka jana  alianza kutoa maombi ya kustaajabisha  hasa wakati wa msimu wa sherehe. Mwangoka  anasema bosi wake alianza kumtaka amkande mwili mzima.

“kilichonishangaza ni kwamba angeniita katika chumba cha kumkanda na ningempata akiwa uchi wa mnyama  amelala kifudifudi  akinitaka nimkande," amesema  Mwangoka.

Hatua yake ya kulalamika ilivutia vitisho vya kufutwa kazi.  Alikubali kumkanda na hata katika sehemu zake siri . Kulingana na Mwangoka  bosi wake  alikuwa akimtaka alitumie bomba la maji   pamoja na sabuni ya mwarubaini ili kumsafisha mkondo wa kwenda  haja kubwa .

“ Baada ya hapo angekwenda chooni kuendesha  kabla ya kurejea na kutaka nimkande tena’ amesema Mwangoka

“ Baada ya hapo jamaa alikuwa akirusha mashuzi makali yenye harufu ya kumwangamiza hata mende. Nilihofia angeniambukiza ugonjwa usiojulikana".

Alitumia fursa ya ukarimu wake kuitisha mkopo wa shilingi 8000  alizotumia kununua simu za kisasa ili kuweza kuchukua picha za vitendo hivyo kama ushahidi. Afisa kutoka shirika la Muhuri Francis Auma anasema kisa hicho ni tukio halisi la dhulma za kimapenzi.

Tukio lenyewe limeripotiwa katika kituo cha polisi cha Central   chini ya nambari OB 33/21/01/2020. Auma  amesema visa vya dhulma za kimapenzi Mombasa vimeongezeka hasa katika mitaa ya   Kizingo, Nyali  na Tudor.

“ Maeneo haya ya kifaharai yana usiri mkubwa. Polisi hawapigi doria katika mitaa hii kwa sababu ni ya watu mashuhuri na wenye uwezo mombasa ambao wanazingatia sana usiri na mambo yao",  alisema Auma .

Amewahimiza polisi kukichunguza kisa kilichomfika Mwangoka na kumkamata bosi wake .

  “ watu wengi hasa wafanyikazi wa nyumbani wanapitia mateso haya kimya kimya  kwa sababu wanahisi hakuna wanachoweza kufanya". Amesema Auma.
Mwaka jana shirika la Muhuri lilisema kwamba lilisajili visa 20 vya dhulma za kimapenzi  na dhulma za kijinsia.  Auma anasema  kuna raia wengi wa kigeni hasa watanzania na Waganda wanaopitia mateso mbali mbali katika majumba ya kifahari katika eneo la Mombasa kwa sababu waliingia nchini Kenya kwa njia isio halali .
“ Huko Magongo kwa mfano, kuna raia wengi wa Uganda  hasa wanawake  wanaofanya kazi katika mabaaa ambao hudhulumiwa kimapenzi kila siku  lakini hawawezi kuripoti kwa sababu wanazihitaji kazi hizo," Amesema afisa huyo.
Polisi wamesema watakichunguza kwa kina kisa cha Mwangoka na kuchukua hatua zifaazo.