‘KDF walijificha ‘ kichakani wakati wa shambulizi la Manda Bay-Amerika yasema
Wamarekani wamewakosoa wanajeshi wa KDF kuhusiana na mienendo yao wakati wa shambulizi la al shabaab katika Camp Simba huko manad bay januri tarehe 5 . Kulingaana na gazeti la the , wanajeshi wa Kenya walijificha kwenye majani wakati wa shambulizi hilo lilopelekea kuuawa kwa wamarekani watatu .
" wanajeshi wengi wa Kenya waliopewa jukumu la kuilinda kambi hiyo walijificha kwenye nyasi wakati wanajeshi wa marekani na wafanyikazi kadhaa walipokuwa katika mahema yao wakingoja vita kutamatika’ gazeti ya NYT limeandika . Ufichuzi huo henda ukazua lalama kutoka kwa serikali ya Kenya na KDF kwa ajili ya athari zake kuwachafulia sifa na jina wanajeshi wa humu nchini . Mwanajeshi mmoja wa Amerika na raia wawili waliokuwa wanakndarasi waliuawa katika shambulizi hilo la al shabaab .
Wanajeshi wengine wawili wa Marekani walijeruhiwa katika shambulizi hilo . Gazeti hilo la Amerika pia limeonekana kuashiria kwamba huenda wafanyikazi wa kenya katika kambi hiyo waliwasaidia wapiganaji wa Al shabaab . Gazeti hilo limesema Kenya ilitangaza kuwakamata washukiwa sita wa al shabaab lakini baadaye ilibainika kwamba walikuwa wapita njia ambao baadaye waliachiliwa huru .