Akothee atishia kumnyoa mpenzi wa binti yake, Rue
Esther Akoth almaarufu Akothee hajafurahishwa na mtindo wa nywele wa mmoja wa wacheshi wa Kenya ambaye ana uhusiano na bintiye Rue kwa muda sasa.
Akothee ametishia kumnyoa 'mkwe wake' na kumtaka bintiye Rue kufikisha ujumbe.
Lakini ni nini kilicho sababisha rais wa kinamama kusema maneno haya? Hii ni baada ya Akothee kumuuliza mwanawe Rue baby vile mpenziwe ambaye ni 'comedian' alivyokuwa anaendelea.
Akothee alisema kuwa anataka kunyoa mcheshi huyo nywele zake.
Katika ukurasa wake wa Instagram Akothee aliweka video akimshauri Rue kwamba kama anataka mpenzi au mchumba anapaswa kutafuta mwanamume ambaye hana nywele kama za msanii huyo kwa sababu watu wenye mitindo ya nywele kama hiyo ni wasumbufu sana.
"Mpenzi wako anaendelea aje? kwanini unakasirika na kupatwa na hisia hizo ama junadhani sijui," Aliuliza Akothee.
Katika matamshi yake Akothee alimwambia mwanawe kuwa kama anataka kuwa katika uhusiano lazima mpenzi wake anyoe.
La sivyo atakuwa anaitisha pesa za kusongwa mara mbili .