26 January 2020 1 Min Read
Pombe ya Bure:Jamaa wakimbilia kupora pombe baada ya lori la kubeba vileo kuanguka
by Yusuf Juma Habari
Msiba wa mwenzio usiufurahie –lakini jumapili watu kadhaa walikiuka kauli hiyop kwa kumbilia kupora chupa za pombe wakati lori moja la kusafirisha vileo kuanguka katika mzunguko wa westlands
Abiria ,wachuuzi na wahudumu wa matatu walikimbilia pombe hiyo iliyotapakaa baada ya ajali kutokea wakati dereva wa lori hilo alipopoteza mwelekeo na kusababisha gari hilo kuanguka . Hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo .
" Hakuna watu wengi na nashangaa mbona polisi wametuzuia kuichukua pombe hii’ mtu mmoja aliyenufaika na pombe hiyo ya bure alisema . Polisi hata hivyo walifaulu kuokoa kreti kadhaa za pombe hiyo walipowasili katika eneo la mkasa .