Lucy ndiye aliyetuma ujumbe akiomba apatanishwe na mpenziwe bwana Julius.

"Julius ni mpenzi wangu na mwezi uliopita alisema anataka kuja kwangu na nikamwambia angoje nitamwambia. Mda mchache akaniambia yuko karibu na kwetu na anataka tupatane na sikuelewa." Alisema

Isitoshe Lucy anadai kuwa anajua mpenziwe Julius ana mke lakini hilo halimshtui. Hata hivyo anasema kuwa anashuku mpenziwe ana wapenzi wengine wawili.

Kuna Doris Kuna mimi na mke mwingine kwa jina Lucy. Mimi na yeye tuna mtoto mkubwa wa darasa la tatu na mke wake hana habari. Licha ya hayo bado nampenda.

Lucy ana miaka 24 na mpenziwe ana miaka 44.

Ata awe mzee aje Sitaki kujua Kwani nampenda sana.

Alipopigiwa simu Julius alikata mawasiliano mara ya kwanza kabla ya kumshauri Lucy ampigie simu wasuluhishe mambo yao ila si hewani.

Gidi hakuwa hapo tukipatana tafadhali nipigie simu usifanye hii maneno iwe public. Bado tuko pamoja kama Jubilee na mambo ya Doris yaliisha.