ambulance

Serikali ya kaunti ya Kajiado imewasimamisha kazi  wafanyikazi wake wawili baada ya mwanamke mmoja kuaga dunia kwa kujirusha kutoka ambulansi wakati mtoto wake  alipofariki .  Mwanamke huyo aliyetambuliwa kama  Naiso Leslie aliichukua hatua hiyo wakati mtoto, Solomon Lesie, alipoaga dunia akikimbizwa kwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Kajiado .  Miili yao  imepelekwa katika  hifadhi ya maiti ya hospitali hiyo ilhali ambulansi iliyohusika katika tukio lenywewe imekokotwa hadi katika kituo cha polisi cha Kajiado .

  

 Waziri wa afya wa kaunti Esther Somoire  amethibitisha kwamba dereva na muuguzi waliokuwa katika zamu wakati w atkio hilo ndio waliosimamishwa kazi . OCPD wa Kajiado central Daudi Loronyokwe  amesema wawili hao tayari wameandikisha taarifa na polisi huku uchunguzi kuhusu kisa hicho ukiendelea .

Mvulana  aliyeaga dunia alikuwa amelazwakatika kituo cha cha afya cha Bisl  kabla ya kupendekezwa ahamishwe katika hospitali ya rufaa ya kajiado .Kulingana na OCPD ,mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 26 aliufungua mlango wa nyuma wa ambulansi na kuruka nje wakati gari hilo likiwa katika mwendo wa kasi .

View Comments