- Screenshot-from-2020-01-30-06_17_56
- Screenshot-from-2020-01-30-06_05_30
- Kobe-and-family-696x418

Mke wa mchezaji gwiji wa mpira wa vikapu mwendazake Bryant Kobe liweza kuongea kwa mara ya kwanza baaada ya ajali ya helikopta iliyotokea na kuchukua maisha ya mumewe na bintiye juma pili.

Vanessa Bryant kupitia kwa mtandao wa kijamii aliandika ujumbe kwa uzuni huku akimsifia mume wake na bintiye.

Mwanamke huyo aliyevunjika moyo baada ya ajali hiyo aliandika ujumbe katika mtandao wake wa kijamii wa instagram na kusema vile maisha yameweza kubadilika baadda ya kifo cha bintiye na mumewe.

" Mimi na wasichana wangu tunataka kuwashukuru watu wote ambao wameungana nasi kwa maombi na hata kutuma rambirambi zao, kwa kweli tunazihitaji kwa kweli tumeweza kuharibiwa na kushtuka kwa ajili ya ajali hii ya punde,

"Nimeweza kumpoteza mume mzuri na baba wa watoto wangu, na pia binti yangu nimpendaye, aliyekuwa mwenye maarifa, mwenye kupendeza na dada mzuri kwa ndugu zake," Aliandika Vanessa.

Vanessa na Byant walioana mwaka wa 2001 alipokuwa na miaka, 17, na mumewe Kobe alikuwa na miaka, 22, huku akisema walikua wazazi wenye mfano mwema kwa wanao.

"Sina maneno ya kutosha kueleza uchungu na maumivu yetu kwa sasa, nina faraja kuona Kobe na binti yangu Gigi walikuwa wanapendwa sana,

"Kwa hakika tulikua tumebarikiwa kuwa na wao katika maisha yetu, ningetaka tuwe na wao maishani milele, ninaweza kusema kuwa walikuwa baraka kwetu,

"Baraka ambazo zimechukuliwa kwa haraka kutoka kwetu," Alieleza.

Waliweza kuuliza faragha ili waweze kuwaomboleza wawili hao, huku akiandika,

"Sijui maisha imetuekea nini baada ya kupoteza mume wangu na binti yangu, sijui tutaweza kuishi aje bila ya hao wawili,

" Kila siku huwa tunaamka tunaendelea na maisha kwa maana najua Kobe na Gigi wanatuangalia wakiwa mbinguni,

"Ndio maana nasema upendo wetu kwao hauna mwisho wala haupimiki, natamani ningewakumbatia, kuwapa busu na kukaa nawao milele," Vanessa Alisema.

Vanessa, 37, alichukua nafasi hiyo na kutuma rambirambi zake kwa familia za watu ambao waliangamia katika ajali hiyo.

"Nachukua nafasi hii kutuma rambirambi zangu kwa familia ambazo ziliwapotea watu wao, na tuko pamoja kwa wakati huu mgumu," Alisema.
View Comments