Waititu

Ferdinand Waititu sio mgeni wa  masaibu  kama yaliyomkumba jana wakati senate ilipoidhinisha hoja ya kumwondoa afisini kama gavana wa Kiambu . Taaluma yake nzima kisiasa imekuwa na milima na mabonde kama hayo na  wengi watamuangazia kwa karibu kuona hatua zipiz atakazochukua na vipi atajirejesha tena katika ulingo wa kisiasa . Sarakasi zake wakati wa kipindi kizima cha uongozi wake katika nydhfa mbali mbali zimesalia katika kumbukumbu za wengi na    miaka mitano iliyopita hakuna aliyeweza kutabiri kwamba wakati mmoja angeeweza kuwa gavana wa Kiambu ,lakini Waititu ni ‘Baba yao’ kama jina lake . Waititu alianzia mbali na safari yake inasoma hivi .Mwanzo alikuwa diwani katika  serika ya jiji nyakati hizo na baadaye madiwani wenzake walimteua kuwa naibu Meya . Waititu aliwakilisha wadi ya Njiru wakati huo .Baadaye aliwania kiti cha  ubunge cha  Embakasi na kuliwakilisha eneo hilo kwa muhula mmoja . Kisha baadaye alihamia Kabete ili kuwa mbunge baada ya kuuawa kwa mbunge wa eneo hilo George Muchai .

Waititu alizaliwa januari tarehe 1 mwaka wa 1962  na safari yake katika siasa ilianza mwaka wa 2002  alipchaguliwa diwani wa Njiru  kupitia chama cha KANU .  Katika uchaguzi mkuu wa 2007 aliamua kuwania ubunge Embakasi  dhidi ya  kigogo  David Mwenje na  mwanasiasa  aliyekuwa mgeni  kwa siasa za eneo hilo Meritus Mugabe .  Katika uchaguzi huo  Mugabe Were aliwashinda Waititu na Mwenje lakini kwa bahati mabay akauawa katika tukio la wizi nje ya lango lake mtaani Woodley hata kabla ya kuapishwa  januari tarehe 29 mwaka wa 2009 .

Katika uchaguzi mdogo ulioafuatia  Waititu alinyakua ushindi na kateuliwa kuwa  wazri msaidizi katika serikali ya muungano .Baadaye alipokonywa wadhfa huo baada ya  kukabiliwa na madai ya uchochezi  . Mwaka wa 2013 Babayo aliamua kuwania kiti cha ugavana jijini Nairobi kupitia tiketi ya TNA  lakini akashindwa  na  Evans Kidero wa ODM .Wenzake katika kundi la TNA  Mike Sonko na Rachael Shebesh waliushinda viti vya Seneta na mwakilishi wa akina mama mtawalia . Mapema mwaka wa 2015 aliwashangaza wengi alipotangaza kwamba sasa atahamia Kiambu ili kuwania kiti cha eneo bunge la Kabete baada ya kuuawa kwa mbunge wa eneo hilo George Muchai . Alishinda kiti hicho katika uchaguzi mdogo na akapata ujasiri sasa wa kupiga hatua nyingine .Alitangaza kwamba atawania ugavana ili kumbandua  Gavana wa kwanza wa Kiambu William Kabogo .Kabogo alimpuuza kama mtu asiyeweza kumpa ushindan wala kumtoa kijasho lakini  Babayao alipombwaga katika uchaguzi wa mchujo kuwania tiketi ya chama cha Jubilee , tayari guu lake moja lilikuwa katika afisi ya gavana .

Hakupata pumzi  Waititu kwani pindi tu baada ya kuapishwa kama gavana ,tofauti ikaibuka kati yake na naibu wake James Nyoro na washirika wake  kadhaa waliomsaidia kukishinda kiti hicho .Patashika ya hapa na pale  na mgogoro wa uongozi pamoja na vita vya ndani kwa ndani hatimaye vilimzidi maarifa Babayao.Masaibu yake yaliwekwa mafuta yamtelezeshe vizri wakati waakilishi wa kaunti ya Kiambu walipopitisha hoja ya kumfurusha kwa tuhuma za kujinufaisha kutumia kandarasi ,utumizi mbaya wa fedha za umma na kutumia vibaya maamlaka ya afisi yake .Babayao alipewa fursa kufika senate ili kujitetea dhidi ya madai hayo.Aliwaraia maseneta kumsaza na hata akaawambia siku moja watakuwa magavana na  yeye atakuwa seneta kwa hivyo wamhurumie lakini ng’o! Kauli ikawa kumwondolea jina la gavana na kumrejesha katika meza ya kujipanga upya . Hayajaishia hapo-Waititu yungali ana kesi ya kujibu kortini kuhusu madai yaliyotolewa na waakilishi wa kaunti ya Kiambu .

View Comments