HIJACKED:Duale asema Wanasiasa wameuteka nyara mchakato wa BBI .
Kiongozi wa walio wengi bungeni Aden Duale amesema mikutano ya sasa ya ushauriano kuhusu BBI imetekwa nyara na wanasiasa . Mbunge huyo wa Garissa Township amesema ni jambo la kufadhaisha kwamba mchakato uliokuwa na nia njema sasa umetwaliwa na wanasiasa ili kuendeleza maslahi yao . mbunge huyo ametaja mikutano inayofanywa ya BBI katika sehemu mbali mbali za taifa kama ‘inayokanganya’.
“ BBI iliyoanzishwa na rais Kenyatta ilifaa kuwahusisha wakenya wote . ni jambo la kusikitisha kwamba sasa wanasiasa wameutakanyara utaratibu mzima na kusababisha mgawanyiko hata zaidi’ Duale amesema .Duale, ambaye hajahudhuria mkutano wowote wa BBI ameshikilia kwamba hana mpango wa kuhudhuria mkutano wowote wa BBI isipokuwa inayohudhuriwa na naibu wa rais William Ruto na rais Uhuru Kenyatta.
“ kwa sasa nimejawa na majukumu ya bunge linalorejelea vikao vyake wiki ijayo .watu wa kaskazini mashariki mwa nchi wana matatizo mengi kama vile ukosefu wa usalama ,kufungwa kwa shule na suala la sensa .Haya ndio masuala ninayoyazingatia kwa sasa ‘ amesema Duale . Matamshi ya Duale yanajiri siku moja siku mbili tu baada ya rais Uhuru Kenyatta kusema kwamba mikutano ya BBI inayoendelea katika sehemu mbali mbali za nchi hailengi kumtenga yeyote .