Msilete ghasia katika BBI-Ruto atoa rai baada ya vurugu za Kitui
Naibu wa rais William Ruto amekashifu ghasia zilizoshuhudiwa siku ya jumamosi wakati wa mkutano wa BBI huko Kitui . Ruto amesema hakuna utangamano na umoja unaoweza kuafikiwa kutumia ghasia akisema kila mkenya ana hakika ya kusikizwa . “ sasa sio wakati wa kujigamba ,kupiga kifua na kuchukua misimamo mikali’ amesema Ruto katika shule ya wasichana ya Itoerio huko Kisii ." tufanye kazi kwa pamoja na tuvimiliane ili tuweze kusikilizana . hata walio wanyonge wana jambo la kusema . mjadala huu sio wa viongozi au wanasiasa pekee’ amesema Ruto.
Miongoni mwa viongozi waliomkaribisha Ruto na kuapa kumuunga mkono katika uchaguzi mkuu ujao ni pamoja na naibu gavana wa Kisii Joash Maangi ,wabunge Silvanus Osoro (South Mugirango) na Alpha Miruka (Bomachoge Chache). Siku ya jumamosi kulikuwa na rabsha katika mkutano wa BBI huko Kituo ambapo baadhi ya washirika wa Naibu wa rais walihangaishwa na watoa ulinzi pamoja na baadhi ya waliohudhuria mkutano huo.
Wabunge waliowasili baada ya mkutano huo kuanza walizuiwa kufika jukwani ambapo kiongozi wa ODM Raila Odinga alimywa ameketi pamoja na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka ,magavana na viongozi wengine walioachaguliwa . Zaidi watu 40 wa kutoa ulinzi waliwavizia na kuwazuia viongozi wa tanga tanga wakiwemo Kipchumba Murkomen (Elgeyo Marakwet) na seneta wa Kericho Aaron Cheruiyot dhidi ya kufika jukwani . Moses Kuria pia aliyapitia masaibu kama hayo alipofurushwa kutoka mkutano huo .