Shule ya msingi ya kakamega hatimaye imetoa majina ya wanafunzi 14 walioafariki katika tukio la mkanyagano shuleni humo siku ya jumatatu . Mmoja wa waathiriwa hao  mwanafunzi wa gredi ya nne  Naila Kiverenge – anazikwa  jumatano alasiri . Matayarisho ya maazishi yaw engine yanaendelea  baada ya kuundwa kwa kundi  lililoundwa na gavana wa kakamega Wycliffe  Oparanya .

Waathiriwa wengine wa  13 wa kisa hicho  wanatarajiwa kuzikwa wiki ijayo. Serikali kuu na ya kaunti zimeahidi kuzisaidia familia za waathiriwa . huduma za ushauri zinatolewa kwa familia hizo na wanafunzi walionusurika mkasa huo . shule hiyo hata hivyo imefungwa baada ya tukio hilo ambalo limeishangaza nchi . Orodha kamili ya waathiriwa wote ambao mmili yao ilitambuliwa na jamaa zao katika  Hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa ya Kakamega ni hii

  1. Antonnet Iramwenya – 5V

    2. Prudence Eliza – 5V

    3. Catherine Aloo – 5W

    4. Naila Kiverenge – 4G

    5. Prince Vermaline – 4G

    6. Nichole Achola – 5P

    7. Venessa Adesa – 5P

    8. Fidel Kumbetie – 5P

    9. Simon Waweru – 4G

    10. Samuel Simekha – 5V

    11. Lavenda Akasa – 5P

    12. June Nakhumicha – 4G

    13. Joseph Musami – 5B

    14. Bertha Munywele – 5Y

View Comments