Bwana Ken aliomba ndoa yake iokolewe katika kitengo cha leo cha patanisho.

Nina mke na watoto wawili ambao niliingia kwa ndoa nao baada ya mke wake wa kwanza kuondoka na kumuachia watoto. Sasa siku moja ikiwa Jumapili, aliondoka tu ghafla na kubeba vyeti vyake vya shule na kuondoka, sasa hivi naskia kuwa yuko kwa dadake. Alijieleza Ken.

Aliongeza,

Sasa ningependa kuzungumza naye ili nijue shida ilitoka wapi kwani sikumkosea.

Ken anasema kuwa wawili hao walijaribu kupata mtoto ila walimpoteza mtoto wao kabla ya kujifungua. Isitoshe aliongeza kuwa mpenziwe anawapenda watoto wake na hana tashwishi lolote nao.

Alipopigiwa simu bi Roseline alisema kuwa mumewe anajua chenye alifanya ili kumkosea akidai kuwa Ken alipaswa kujenga lakini alichelewa na hilo likamfanya aondoke.

Hata kama sijazaa naye, niliwachukua watoto wake kama wangu. Kuna wakati tulikuwa kwa mkutano na akasema ifikapo Januari atakuwa amejenga na hapo nikaona maji yamezidi unga na nikaondoka.

Aliongeza kuwa Ken alikuwa amemwambia atamleta Patanisho na kumwambia kuwa hatishiki.

Kwa upande wake, Ken alijitetea akidai kuwa mambo hayakuwa tayari lakini sasa hivi yuko tayari kuanza mikakati ya ujenzi.