Mawazo na Kukosa pesa: Dakika za mwisho mwisho kabla Papa Dennis kujirusha
Msanii wa Gospel Papa Dennis huenda alikuwa na mawazo kupindukia na matatizo ya kukosa pesa ,jamaa yake ,rafiki na msimamizi nyumba alikokuwa wamesema .
Majirani na msimamizi wa nyumba alioishi Dennis wamesema nyoashukuru’ aliyepatikana amefariki siku ya jumamosi alikuwa matatizo ya hela na huenda yalichania hatua yake kujiua .
“ Mwenye nyumba ALIKOISHI MTAANI JAMHURI ALIKUWA AMEMFUNGIA NYUMBA NA WATU ALIOKUWA AKIISHI NAO KWA MUDA WALIKUWA WAKIMPIGA . HAPO NDIPO MMILIKI WA STUDIO ILIYOKO JENGO LA KIRIMA ALIMTAKA AJE AISHI HUKO KWA MUDA AKITULIZA FIKRA ZAKE' Jamaa yake wa karibu amesema
Papa Dennis pia inaripotiwa alikuwa na matatizo na mpenzi wake wa miaka miwili ambaye ni muigizaji katika kipindi kimoja cha televisheni humu nchini .
“ Siku ya ijumaa mwendo wa saa tano asubuhi papa dennis alimpigiasimu mjukuu na kumwambia kwamba kuna waliokuwa wakipigana katika nyumba iliyo na studio’ msimamizi wa nyumba hiyo amesema .
“ Mmiliki wa studio alinipia simu na nilipobishamlango ,Dennis ndiye alaiyefungua’
Msimamizi huyo wa nyumba amesema baadaye Dennis alichukua simu yake na kupanda pikipiki akielekea upande wa Muthaiga katika barabara ya Thika .Papa Dennis alirejea baadaye na kakake pacha Simon Mwangi akajiunga naye na producer ili waendelee kurekodi katika studio hiyo .
“ Kisha aliichukua simu yake na chaja katikati ya kurekodi na kutoka akisema kakake na producer walikuwa wakimpa wakati mgumu’. Msimamizi huyo wa nyumba baadaye siku ya ijumaa aliarifiwa na baadhi ya wapangaji kwamba kuna mtu aliyeruka kutoka upande wa pili wa jingo kutoka ghorofa ya nne .“ Nilimuambia kakake na maneja wa studio na mmiliki wa studio kwamba mmoja wa rafiki yao ameruka kutoka ghorofa ya nne’ msimamizi huyo amesema .
“ Hatuna uhakika wa jinsi alivyofika upande wa pili wa mwisho wa kabisa wa jingo hilo kwa sababu milango yote ya kwenda upande huo ilikuwa imefungwa . chaguo jingine na kupitia nyumba ya mtu au kupitia paa ,jambo ambalo ni gumu’ msimamizi huyo amesema .