Rais Uhuu Kenyatta na mkewe Margaret wautazama mwili wa Mzee Moi

Mwili wa marehemu Mzee Daniel Moi  ulivalishwa suti tofauti kila siku ambayo ulipelekwa bungeni kutazamwa na wananchi .

  Siku ya jumatatu ambayo ndio ya mwisho mwili huo kuwekwa katika majengo ya bunge ili kutazamwa na umma , mwili wa Moi ulivalishwa  suti ya rangi ya kijivu (grey) ,viatu vya  rangi ya  kahawia(brown) ,shati jeupe na  tai yenye vistari vya  manjano . Kirungu kidogo cha mzee Moi al maarufu fimbo ya nyayo  kiliwekwa katika mkono wake wa kulia kinyume na siku mbili za awali ambapo kiliwekwa kando yake . Siku ya kwanza ya kuutazama mwili huo jumaosi  ,ulivalishwa  suti ya  rangi ya kijivu  shati jeupe na viatu vya  rangi ya kahawia  na tai yenye maua . Siku ya jumapili iliyokuwa ya pili kwa mwili wake kutazamwa na umma ,alivalishwa  suti nyeusi ,shati jeupe ,tai ya rangi nyekundu na  viatu vyeusi .

 

 Viongozi ambao tayari wameuona mwili wa Mzee Moi ni pamoja na rais Uhuru Kenyatta ,naibu wake William Ruto ,rais mstaafu  Mwai Kibaki ,mabalozi ,wabunge  na maseneta,magavana na viongozi wa kidini .

Rais huyo wa zamani atapewa taadhima zote za kijeshi   wakati wa maazishi yake ikiwemo saluti ya milio 19 ya risasi . Siku ya jumanne misa ya madhehebu mbali mbali itafanyika katika uwanja wa Nyayo Nairobi . Moi atazikwa nyumbani kwake Kabarak siku ya jumatano .

 

View Comments